1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Guterres alaani shambulio la anga lililowaua watu 22 Sudan

Sylvia Mwehozi
9 Julai 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio la anga ambalo linaripotiwa kuwaua watu 22 nchini Sudan siku ya Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4TdRI
Uharibifu wa jengo mjini Omdurman
Picha ya jengo lililoharibiwa kwenye mapigano ya SudanPicha: Mostafa Saied/REUTERS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio la anga ambalo linaripotiwa kuwaua watu 22 nchini Sudan siku ya Jumamosi.

Naibu msemaji wake, Farhan Haq amesema kuwa Katibu Mkuu Guterres pia amesikitishwa na taarifa za kuongezeka kwa ghasia na majeruhi katika mkoa wa Darfur.

Wizara ya afya ya mjini Khartoum ilisema katika taarifa yake kwamba takribani watu 22 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Sudan katika mkoa wa magharibi wa Omdurman. Pia kumeripotiwa mapigano mapya katika majimbo ya Kordofan Kusini na Kaskazini na jimbo la Blue Nile.

Mapigano ya Sudan baina ya mkuu wa kijeshi Abdel Fatah al Burhan na aliyekuwa makamu wake Mohammed Hamdan Dagalo sasa yameingia wiki ya 12.