1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGuinea

Guinea yasema udhibiti wa mtandao ni muhimu kwa "usalama"

11 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea amewaambia wanadiplomasia kwamba udhibiti uliowekwa juu ya upatikanaji wa huduma ya intaneti katika taifa hilo la Afrika Magharibi ulikuwa unahitajika kwa sababu ya tatizo la kiusalama.

https://p.dw.com/p/4b8fT
Conakry Mji Mkuu wa Guinea
Conakry Mji Mkuu wa GuineaPicha: picture alliance/dpa/MAXPPP

Takribani mabalozi 15 au wawakilishi, wakiwemo kutoka Umoja wa Ulaya, Marekani na China, walikutana na waziri huyo kuelezea wasiwasi wao juu ya kukatwa kwa huduma hiyo, kulingana na taarifa iliyorushwa na kituo cha televisheni ya serikali.

Walitaja vizuwizi vinavyoikabili Guinea ikiwa ni pamoja na juu ya uhuru wa kujieleza na upatikanaji wa intaneti, uhaba wa mafuta na moto mbaya ulioikumba bohari kuu ya mafuta mwezi Desemba, pamoja na vikwazo kwa wafanyakazi wa ofisi zao.

Kwa wiki kadhaa sasa, upatikanaji wa intaneti umepungua sana katika nchi hiyo ambayo inatawaliwa na viongozi wa kijeshi walioingia madarakani kupitia mapinduzi ya mwaka 2021.

Waziri wa mambo ya nje amewaambia wanadiplomasia hao kuwa matatizo yanayozikumba balozi zao yamezikumba pia wizara za Guinea, na kwamba hata ofisi ya rais inakabiliwa na matatizo ya mtandao, huku akiahidi kwamba yatatatuliwa haraka iwezekanavyo.