1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guardiola: sioni shida kufanya mbili kwa sasa

6 Februari 2016

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola anasema hatua yake ya kujiunga na Manchester City ya Uingereza msimu ujao, haitaathiri kazi yake katika kilabu ya Bayern Munich msimu huu.

https://p.dw.com/p/1HqnA
Fußball Bundesliga Hamburger SV - FC Bayern München Trainer Josep Guardiola
Picha: picture-alliance/dpa/S. Sudheimer

Guardiola mwenye umri wa miaka 45, alisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuchukua mikoba ya Manuel Pellegrini mwishoni mwa msimu huu.

Alipoulizwa ikiwa itakuwa kazi ngumu kwake hivi sasa, Guardiola alijibu, ''Kwa nini vigumu? Mimi ni kama mwanamke, naweza kufanya kazi mbili mara moja na kudhibiti hali zote mbili. Nina kipaji kikubwa katika hili.''

Guardiola mwenye umri wa miaka 45, atajiunga na makocha walio na umri wa miaka arubaini na kitu nchini England ambao wanaheshimika sana, wanaomjumuisha Jurgen Klopp wa Liverpool, Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspurs.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Josephat Charo