1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghana yashindwa kufuzu fainali ya AFCON mwakani

Sylvia Mwehozi
16 Novemba 2024

Ghana imeshindwa kufuzu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Angola.

https://p.dw.com/p/4n44B
mashabiki wa Ghana
mashabiki wa GhanaPicha: picture-alliance/dpa/Tuggela Ridley

Ghana imeshindwa kufuzu fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Angola.

Timu hiyo maarufu kama Black Stars ilihitaji ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ili kufufua matumaini yao madogo ya kufuzu fainali ya michuano hiyo nchini Morocco hapo mwakani.

Mabingwa hao mara nne wa Kombe la Afrika, wameshiriki michuano hiyo kwa mara 24. Angola ambayo tayari imefuzu ilianza vema mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa nyumbani wa Talatona.Ghana huenda ikashindwa kufuzu fainali ya Kombe la Mataifa Afrika

Katika mechi nyingine Zambia, Mali, na Zimbabwe zimefuzu mapema Ijumaa, huku Nigeria, Tunisia, Afrika Kusini, Uganda, Guinea ya Ikweta na Gabon nazo zikikata tiketi siku ya Alhamisi.