1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Viongozi wa Israel na Palestina wanasema yapo matumaini ya kuanzishwa tena mazungumzo ya amani

27 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCp3

Viongozi wa Israel na Palestina wamesema kwamba makubaliano ya kusimamisha mashambulio katika eneo la Ukanda wa Gaza yatawezesha kurejelewa tena mazungumzo ya amani baina ya pande hizo mbili.

Katika siku ya kwanza ya makubaliano hayo hata hivyo kumetokea mashambulio ya makombora kutoka ukanda wa Gaza kulekezwa ndani ya ardhi ya Israel katika masaa machache tu baada ya kuanza rasmi amri ya kusimamisha mashambulio.

Makundi mawili yenye msimamo mkali ya upande wa Palestina ya Hamas na Islamic Jihad yamedai kuhusika na mashambulio hayo.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema kwamba amewataka makamanda wa majeshi ya Israel kuwa na subira na kutojibu mashambulio hayo.

Waziri mkuu wa Palestina Ismail Haniya nae amesema kwamba makundi yote makubwa katika ardhi ya Wapalestina yamekubali kusimamisha mashambulio dhidi ya taifa la Kiyahudi.

Wakati huo huo Israel pia imeahidi kuyaondosha majeshi yake kutoka ukanda wa Gaza.