1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Spika wa bunge la Palestina apelekwa hospitalini

8 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDNk

Spika wa bunge la Palestina, Aziz Dweik, aliyekamatwa na wanajeshi wa Israel Jumapili iliyopita katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan, alipelekwa hospitalini hapo jana akiwa na maumivu ya moyo na matatizo ya kupumua.

Msemaji wa Aziz, Baha Youssef, amesema hali mbaya ya afya ya kiongozi huyo imesababishwa na kipigo cha walinzi wa gereza la jeshi la Israel anakozuiliwa, lakini jeshi la Israel limeyakanusha madai hayo.

Dweik alikamatwa kwa kuwa mwanachama wa kundi la Hamas ambalo Israel inalitambua kama kundi la kigaidi.