Freeman Mbowe akubali kushindwa uenyekiti CHADEMA
22 Januari 2025Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amechaguliwa kuwa kiongozi wa Chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo,CHADEMA,katika uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo akimbwaga kiongozi wa muda mrefu Freeman Mbowe.
Lissu alipata ushindi mwembamba katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa CHADEMA.
Mbowe ambaye ameiongoza CHADEMA kwa miongo miwili ampongeza Lissu ambaye kabla ya uchaguzi huo alikuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho.
Soma pia:Lissu ambwaga Mbowe uenyekiti CHADEMA
Mabadiliko hayo ya uongozi yanatokea katikati ya mbinyo unaovikabili vyama vya upinzani kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki pamoja na misuguano ya ndani ya vyama ambayo wachambuzi wanasema inaweza kuteteresha nafasi yao kuelekea uchaguzi unaokuja.
Tanzania itafanya uchaguzi mkuu mnamo mwezi Oktoba ambao utakuwa wa kwanza chini ya Rais Samia Suluhu aliyeingia madarakani mwezi Machi 2021 kufuatia kifo cha