1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Felix aiangamiza klabu yake ya Atletico Madrid

4 Desemba 2023

Barcelona walifanikiwa kupata pointi tatu muhimu dhidi ya Atletico Madrid baada ya kuwalaza moja bila katika mechi ya La Liga, huku Joao Felix, mchezaji wa zamani wa Atletico, akiwa mfungaji wa goli hilo la pekee.

https://p.dw.com/p/4Zlan
Kandanda Uhispania La Liga | FC Barcelona - Athletic Bilbao
Marc Guiu wa BarcelonaPicha: Javier Borrego/AFP7/picture alliance

Kilichowashangaza wengi ni jinsi Felix alivyosherehekea kulifunga bao hilo kama mchezaji ambaye hataki tena kurudi Atletico.

Kwa kawaida mchezaji anapofunga dhidi ya klabu anayoichezea wengi huonyesha heshima kutosherehekea ila mambo yalikuwa tofauti kwa Felix.

Kwa ushindi huo, Barca sasa wanaishikilia nafasi ya tatu katika msimamo wa Bundesliga wakiwa na pointi 34, pointi nne nyuma ya vinara Real Madrid na Girona. Atletico wanaishikilia nafasi ya nne pointi zao zikiwa 31 ila hawajacheza mechi moja.

Vyanzo: Reuters/AFP