1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FBI yachunguza madai ya Iran kudukua kampeni za Trump, Biden

13 Agosti 2024

Shirika la upelelezi la Marekani, FBI, linachunguza kile kinachoshukiwa kuwa majaribio ya udukuzi yanayodaiwa kufanywa na Iran dhidi ya kampeni za wagombea wa vyama vya Democratic na Republican.

https://p.dw.com/p/4jOg5
Udukuzi
Timu ya Kampeni ya Trump iliilaumu Iran kwa udukuzi. Iran inakanusha kuhusika.Picha: Sebastiaan Stam/Unsplash

Shirika la upelelezi la Marekani, FBI, linachunguza kile kinachoshukiwa kuwa majaribio ya udukuzi yanayodaiwa kufanywa na Iran, yaliowalenga washauri wa kampeni ya Democratic ya Rais Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris, na mshirika wa mgombea wa chama Republican Donald Trump.

Gazeti la Washington Post limeripoti jana kuwa uchunguzi huo wa FBI ulianza mwezi Juni, wakati Biden akiwa bado anawania urais, wakishuku kwamba Iran ilihusika na jaribio la kuiba data kutoka kambi za wagombea urais wa Marekani.

Kampeni ya Harris haikujibu ombi za kuzungumzia kadhia hiyo, lakini kampeni ya Trump ilisema mwishoni mwa wiki kwamba Iran ilidukuwa moja ya tovuti zake na FBI ilisema ilikuwa inachunguza suala hilo.

Washington Post imesema wachunguzi hawajapata ushahidi wa kufanikiwa kwa majarbio ya udukuzi dhidi ya kampeni ya chama cha Demokcratic. Iran imekanusha kuingilia uchaguzi wa Marekani.