1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Familia za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopia zadai haki

11 Machi 2023

Familia za wahanga wa ajali ya ndege ya Ethiopia aina ya Boeing 737 MAX ya mwaka 2019, Ijumaa zilikusanyika karibu na makao makuu ya kampuni ya kutengeneza ndege za Boeing kulaani kile walichokiita hali ya kutokujali

https://p.dw.com/p/4OYAd
Unfälle und Zertörungen in Russland
Picha: Alexander Ryumin/dpa/picture alliance

Catherine Berthet aliyempoteza bintiye Camille katika ajali hiyo, amesema hakujafanyika uchunguzi kuanzia wa kimahakama hadi wa kijinai nchini Marekani wa mauaji hayo. Berthet, raia wa Ufaransa, alijumuika na familia nyingine kutoka Canada na Ujerumani na kuonesha picha za wapendwa wao walioangamia huku wakinyeshewa na mvua nje ya makao hayo makuu ya Boeing katika kitongoji cha Virginia.

Mnamo Machi 10 mwaka 2019, dakika sita baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Addis Ababa kueleka Nairobi, Kenya, Ndege nambari ET302 ilianguka na abiria wote 157 pamoja na wafanyakazi kwenye ndege hiyo walifariki dunia.