1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Euro 2024: Je, Portugal watalipiza kisasi kwa Slovenia?

1 Julai 2024

Mechi ya pili ya mtoano Jumatatu itawapatanisha Ureno na Slovenia. Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Frankfurt.

https://p.dw.com/p/4hkBW
Euro 2024 Georgien – Portugal | Cristiano Ronaldo
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano RonaldoPicha: Leon Kuegeler/REUTERS

Ureno wanaingia katika mechi hii wakiwa walifungwa katika mechi yao iliyopita dhidi ya Georgia ila kocha wao Roberto Martinez aliyekibadilisha pakubwa kikosi chake katika mchuano huo anasema, vijana wake watakuwa tayari kuvaana na Slovenia.

Martinez anasema wanastahili kujichunga na hao wapinzani wao wa leo kwani ni mojawapo ya timu zenye safu nzuri za ulinzi katika mashindano haya ya Ulaya.

Ikumbukwe kwamba Slovenia waliilaza Ureno 2-0 katika mechi ya kirafiki na Martinez anasema kuwa anamheshimu sana kocha Matjaz Kek. Mshindi wa mechi hii ya mtoano atakuwa anapambana na ama Ufaransa au Ubelgiji katika mechi ya robo fainali.

Vyanzo: Reuters/DPAE