1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kuujadili mgogoro wa Azerbaijan na Armenia

2 Juni 2023

Azerbaijan na Armenia zimefanya mazungumzo mara chungu nzima katika miezi ya hivi karibuni kutafuta suluhisho la mgogoro wao.

https://p.dw.com/p/4S6KI
Belgien I Charles Michel in Brüssel
Picha: John Thys/AFP

Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel amesema anataraji mkutano wa kilele wa Umoja huo nchini Moldova utatowa fursa kwa Azerbaijan na Armenia kuonesha dhamira yao ya kutaka kuupatia ufumbuzi mgogoro kati ya nchi zao.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Urusi Tass Michel,pamoja na waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan watakutana mwezi Julai mjini Brussels.

Aidha shirika hilo la habari limesema  mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili zenye mzozo watakutana mjini Washington Juni 12.

Nchi hizo jirani, Azerbaijan na Armenia zimefanya mazungumzo mara chungunzima katika miezi ya hivi karibuni kutafuta suluhisho la mgogoro wao wa muda mrefu kuhusiana na jimbo la Nagorno-Karabakh.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW