Taifa la kifalme la eSwatini ambalo zamani lilijulikana kama Swaziland linatimiza miaka 50 tangu lijipatie uhuru wake. Mjadala mkubwa uliotawala ni namna nchi hiyo ilivyobadili jina, hali ambayo itailazimu sasa kutumia gharama kubwa kubadili kila kitu ambacho kilikuwa na jina la awali. Sylvia Mwehozi amezungumza na Prof Mwesiga Baregu, ili kufahamu tija ya kubadili jina wakati huu.