1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Enrique ataka vitisho dhidi ya Moratta vikome

28 Juni 2021

Uhispania watakuwa wanapambana na Croatia katika mechi ya kuwania atakayefuzu hatua ya robo fainali ya mashindano ya Euro.

https://p.dw.com/p/3vh8M
Spanien Sevilla | UEFA EURO 2020 | Spanien vs Polen | Jubel 1:0
Picha: David Ramos/AFP/Getty Images

Mechi hiyo imegubikwa na wingu la vitisho alivyopewa mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Moratta na baadhi ya mashabiki wa Uhispania baada ya kukosa nafasi za wazi za kufunga katika mechi zao za duru ya makundi.

Na sasa kocha wa Uhispania Luis Enrique, amewataka maafisa wa polisi wachunguze waliohusika na kumtishia Moratta pamoja na familia yake na hatua zichukuliwe.

"Nafikiri hili ni jambo kubwa na linastahili kushughulikiwa na polisi. Matusi na vitisho vya mauaji kwa mtu yeyote hasa familia na watoto ni kitendo cha uhalifu. Hili ni jambo ambalo serikali inastahili kulishughulikia na kutoa taarifa kulaani kitendo hicho," alisema Enrique.

Euro 2020 | Kroatien Schottland Modric  Tor
Luka Modric akifunga goli dhidi ya ScotlandPicha: Andy Buchanan/REUTERS

Uhispania Jumatatu wanacheza na Croatia mjini Copenhagen, Denmark, na hawatokuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mashabiki kama ilivyokuwa katika mechi zao za makundi walizokuwa wakizichezea mjini Sevilla waliposhinda mechi moja tu.

Croatia watakuwa bila winga wao machachari Ivan Perisic ambaye ameambukizwa virusi vya corona ila matumaini watayaweka kwa nyota ambaye pia ni nahodha wao Luka Modric.