1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Emir wa Qatar aanza ziara barani Ulaya

17 Mei 2022

Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani leo ameanza ziara ya kisrikali nchini Uhispania huku bara la Ulaya likiania kutanua vyanzo vya upatikanaji gesi yasili kupunguza utegemezo wa nishati kutoka Urusi

https://p.dw.com/p/4BQKi
Katar Doha | Staatsoberhaupt des Emirats | Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani
Picha: Qatar Emirate Council/dpa/picture-alliance

Al Thani amelakiwa na Mfalme Felipe VI katika kasri la mjini Madrid, siku ya kwanza ya ziara yake ya siku mbili, ambayo ni kwanza tangu nchini Uhispania tangu aliposhika madaraka mnamo 2013.

Ameandama na waziri wa mambo ya nje na waziri wa nishati. Amepangiwa kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez kesho Jumatano.

Duru ya serikali ya imesema Uhispania na Qatar zinatarajiwa kusaini mikataba kadhaa ya kiuchumi na kibiashara wakati wa ziara hiyo, hususan kuhusu nishati.

Ziara ya kiongozi huyo wa Qatar Ulaya inazijumuisha Ujerumani, Uingereza, Slovenia na Uswisi, ambako atahudhuria Jukwaa la kiuchumi la kimataifa huko Davos kati ya Mei 22 na 26.

Chanzo: ap