1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya tatu ya kubadilishana wafungwa na mateka yakamilika

31 Januari 2025

Duru mpya ya kubadilishana mateka na wafungwa kati ya Israel na Hamas imefanyika jana Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4prJ9
Ukanda wa Gaza Jabalia 2025 | Hamas yamkabidhi mateka wa Israel Agam Berger
Hamas ikimkabidhi mateka wa Israel Agam BergerPicha: Omar Al-Qattaa/AFP

Mabasi yaliyo na wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa chini ya makubaliano ya kusitisha vita yaliondoka kutoka Gereza la Israel la Ofer lililoko Ukingo wa Magharibi baada ya kuchelewa kwa saa kadhaa.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, Wapalestina 66 walipokelewa na jamaa zao. Israel ilitarajiwa kuachilia jumla ya Wapalestina 110 kwa kubadilishana na mateka wanane - wakiwemo Waisraeli watatu na Wathailand watano.

Soma pia: Mateka 4 wa Israel na wafungwa 200 wa Kipalestina waachiwa

Wafungwa waliotolewa walijumuisha 30 waliohukumiwa kwa mauaji, pamoja na wanawake na watoto. Wengine walipaswa kusafirishwa kwenda Gaza, huku wengine wakipelekwa uhamishoni kutokana na uzito wa makosa yao.

Wakati huo, Wapalestina wawili wameuawa katika mji wa Jenin, Ukingo wa Magharibi kaskazini, katika mapigano na vikosi vya Israeli, huku taarifa zikieleza kuwa mwanajeshi mmoja wa Israel aliuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya wakati wa operesheni katika mji huo.