1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Duma yapitisha sheria ya ukomo wa umri jeshini

25 Julai 2023

Wabunge nchini Urusi leo wameunga mkono sheria ya kuongeza kikomo cha umri wa juu hadi miaka 30 kwa huduma ya lazima ya kijeshi, zaidi ya mwaka mmoja tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4UNO0
Russland Moskau Staats-Duma
Picha: The State Duma/AP/picture alliance

Mswaada huo unakuja wakati Urusi inaimarisha vikosi vyake nchini Ukraine bila ya kugeukia uhamasishaji mwingine, hatua ambayo ikulu ya Kremlin ilichukuwa mnamo mwezi Septemba na kuthibitisha kuwa isiyofaa.

Baada ya mswaada huo kupitishwa kwa  kusomwa mara ya pili na tatu, baraza la chini la bunge limesema kuwa kuanzia Januari 1, 2024, raia wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 30, watahitajika kuhudumu katika jeshi.

Soma pia:Wabunge Bunge la Ulaya wataka raia wa Urusi wasaidiwe

Mswaada huo bado utahitaji kupitishwa na baraza la juu la bunge hilo, Duma, kabla ya kutiwa saini kuwa sheria na Rais Vladimri Putin.

Awali, ilikuwalazima kwa wanaume wa Urusiwa kati ya umri wa miaka 18 hadi 27 kuhudumu katika jeshi kwa muda wa mwaka mmoja na usajili kufanywa mara mbili kwa mwaka.