1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yatoka sare ya 1 - 1 na PSV Ligi ya Mabingwa

21 Februari 2024

Borussia Dortmund ililazimika kutoka sare ya bao 1 - 1 na PSV Eindhoven ya Uholanzi katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 za mwisho jana usiku

https://p.dw.com/p/4cdYH
Mallen ni mchezaji wa zamani wa PSV
Mallen alifungia Dortmund dhidi ya timu yake ya zamani PSV ambao walipoteza nafasi nyingiPicha: Rolf Vennenbernd/dpa/picture alliance

Borussia Dortmund ililazimika kutoka sare ya bao 1 - 1 na PSV Eindhoven ya Uholanzi katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 za mwisho jana usiku.

Mshambuliaji wa zamani wa PSV Donyell Malen aliiweka Dortmund kifua mbele katika dakika ya 24 lakini Luuk De Jong akafunga bao la kusawazisha kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 56. Katika mechi nyingine, Inter Milan ya Italia ilipata ushindi mwembamba wa bao 1 - 0 dhidi ya Atletico Madrid.

Marco Arnautovic alitokea benchi la wachezaji wa akiba na kuivunja ngome ya Atletico katika dakika ya 79. Katika mechi za leo, Arsenal watacheza ugenini Ureno dhidi ya Porto wakilenga kufika hatua ya 16 za mwisho za Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza katika miaka saba. Mara ya mwisho The Gunners kutinga robo fainali ilikuwa mwaka wa 2010.

Napoli wanawaalika Barcelonawakilenga kuanza upya msimu wao chini ya kocha wa muda Francesco Calzona. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 aliteuliwa Jumatatu wiki hii kuhudumu hadi mwsiho wa msimu baada ya Walter Mazzarri kufutwa kazi.