1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yatoka sare na Real Madrid

29 Septemba 2016

Borussia Dortmund ilitoka nyuma mara mbili dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya - Champions League Real Madrid na kulazimisha sare ya 2-2

https://p.dw.com/p/2QiGE
Champions League Borussia Dortmund v Real Madrid
Picha: Reuters/K. Pfaffenbach

Cristiano Ronaldo alifungua ukurasa wa mabao kwa upande wa Real katika dakika ya 17 lakini Pierre-Emerick Aubameyang akasawazisha katika dakika ya 43 baada ya kipa Keylor Navas kufanya makosa langoni. Raphael Varane alifungia Real la pili lakini Andre Schuerrle akasawazishia Dortmund zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kukamilika.

Leicester iliizamisha Porto kwa kuifunga bao moja bila kupitia kichwa cha mshambuliaji Islam Slimani na kuchukua usukani wa Kundi G. Copenhagen iliibamiza Brugge mabao manne kwa sifuri katika mchuano mwingine wa kundi hilo.

Katika mechi nyingine, Bayer Leverkusen ilitoka sare ya bao moja kwa moja na Monaco wakati Tottenham Hotspur ilishinda moja bila nyumbani kwa CSKA Moscow katika Kundi E. Sporting Lisbon iliipiga Legia Warsaw mbili bila, Juventus ikaikanyaga Dinamo Zagreb magoli manne kwa bila nao Sevilla wakawashinda Lyon moja bila.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Sekione Kitojo