1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dodoma:Ni nani atakayeshikilia bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu

4 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGq

Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama tawala cha CCM nchini Tanzania katika uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, anatarajiwa kujulikana hii leo. Wajumbe wa mkutano mkuu wataamua kwa njia ya kura kati ya wagombea watatu waliobakia-Dr Salim Ahmed Salim,aliyewahi kuwa waziri mkuu na katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi huru za Afrika na ambaye sasa ni Mwenyekiti wa wakfu wa Mwalimu Nyerere, Waziri wa nje Jakaya Kikwete na Waziri wa mawasiliano na uchukuzi Profesa Mark Mwandosya.