1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Diana Saria: Binti anayehamasisha mabinti kuacha biashara ya ngono

21 Mei 2021

Biashara haramu ya ngono katika jiji la Arusha imekuwa ikiendelea katika eneo hilo la kaskazini mwa Tanzania. Japo kumekuwa na juhudi mbalimbali zinazofanywa za kukomesha biashara hii, imeendelea kushamiri hasa katika miji mikubwa.

https://p.dw.com/p/3tlZo

Kipindi cha Msichana Jasiri kinatazama juhudi za msichana Diana John Saria ambaye amekuwa akiendesha harakati za kuwahamasisha mabinti kuachana na biashara hiyo. Anamudu vipi kufanya kazi hii? Ungana na Veronica Natalis katika makala hii.