1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DARESALAAM: Joto la kisiasa visiwani Zanzibar

6 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFPw

Chama cha upinzani nchini Tanzania kimetangaza kwamba serikali ya Tanzania imetuma kikosi cha polisi pamoja na wanajeshi kuwanyanyasa wafuasi wa upinzani visiwani Zanzibar kabla ya uchaguzi ujao.

Upande wa Upinzani pia umeituhumu serikali ya Tanzania kwa kuandika upya mipaka ya majimbo ya uchaguzi kwa lengo la kudhoofisha mashina ya kura za upinzani.

Naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani CUF Machano Khamis amesema takriban kikosi cha polisi wapatao 60 walivamia nyumbani kwake na kumkamata baada ya kutonywa kwamba anamiliki bunduki kwa njia haramu na kuwaweka majambazi nyumbani kwake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita wafuasi wanaoaminiwa kutoka chama cha CCM walivamia nyumba ya msemaji wa masuala ya fedha katika upinzani CUF na kuichoma moto pamoja na kumpa mkongoto`babake Khamis Said.

Joto la kisiasa visiwani humo limeongezeka huku Upinzani ukitishia kuzusha zogo iwapo chama tawala CCM kitafanya udanganyifu katika uchaguzi wa Oktoba 30.