1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daniel Gakuba

20 Aprili 2017

Mfahamu Daniel Gakuba, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW.

https://p.dw.com/p/2bcsw
Daniel Gakuba
Picha: DW/L. Richardson
  1. Nchi ninayotokea: Rwanda
  2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2011
  3. Nilivyojiunga na DW: Uhusiano wangu na DW ulianza mwaka 2008 nilipokuja Bonn kwa mafunzo ya wiki sita. Kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 nilikuwa mwandishi wa DW mjini Kigali. Kuanzia Agosti 2011 nilijiunga na DW makao makuu mjini Bonn.
  4. Kwa nini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Ilikuwa ndoto yangu ya tangu utotoni na hadi leo ndio chaguo langu la kwanza. Naifurahia sana tasnia hii.
  5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kwanza ni kuipenda kazi hiyo kwa dhati, kisha uisomee. Unaweza pia kuifanya ikiwa umesomea mambo mengine kama lugha, sheria n.k, kisha upate mafunzo maalum kuhusiana na uandishi. Inakubidi kuwa mwelevu anayefuatilia kwa makini mambo ya kitaifa na kimataifa, na uwe na uwezo wa kutofautisha habari sahihi na uvumi, na uwe mwadilifu. Hayo ni baadhi tu.
  6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kuwekewa mpaka na muda; maana yake, muda uliopangiwa kuwasilisha habari ni mfupi ukilinganisha na habari zilizopo ambazo ningependa kuzitangaza. Changamoto nyingine kwa wakati huu, ni mchakamchaka wa kwenda na muda kutokana na teknolojia inayokwenda kasi.
  7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Bila shaka ni mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
  8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Ningependa kumhoji Rais (mstaafu) wa Marekani Barack Obama. Navutiwa sana na haiba yake.