1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAMASCUS: Annan amewasili nchini Syria

1 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDGI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan yupo mji mkuu wa Syria,Damascus.Hicho ni kituo cha mwisho cha ziara yake ya Mashariki ya Kati yenye azma ya kuimarisha usitishaji wa mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.Annan,kabla ya kwenda Damascus alikuwepo Jordan ambako alikutana na Mfalme Abdullah wa Pili.Wote wamesema ni muhimu kutekeleza kwa haraka masharti ya makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliopatikana kupitia Umoja wa Mataifa.Mfalme Abdallah,kama Annan ametoa mwito kwa Israel kuondosha vikwazo vyake dhidi ya Lebanon.