1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Papa Francis anaendelea vizuri baada ya upasuaji wa utumbo

8 Juni 2023

Daktari Sergio Alfieri aliyemfanyia upasuaji Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, amewaambia waandishi wa habari kuwa Papa Francis anaendelea vizuri na kwamba zoezi hilo lilifanyika bila tatizo lolote.

https://p.dw.com/p/4SKSm
Papst Franziskus
Picha: Ettore Ferrari/ANSA/picture alliance

Daktari Sergio Alfieri amesema Baba Mtakatifu atasalia hospitalini hapo kwa siku 5 hadi wiki kwa ajili ya uangalizi. Papa Francis alilazwa siku ya Jumatano katika hospitali ya Gemelli mjini Roma, ili kufanyiwa upasuaji wa utumbo miaka miwili tangu alipopata maradhi yaliyolazimisha madaktari kuondoa sehemu ya utumbo wake mkubwa. Katika miezi ya karibuni, hali ya afya ya kiongozi huyo wa kidini limekuwa suala la mjadala hususani juu ya uwezo wake wa kimwili wa kuendelea kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki lenye zaidi ya waumini wapatao bilioni 1.2 duniani.