1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR.Serikali za Ufaransa na Senegal zatia saini makubaliano ya kudhibiti uhamiaji haramu

25 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD97

Serikali ya kihafidhina nchini Ufaransa imetia saini makubaliano na serikali ya Senegal yatakayolenga kudhibiti ongezeko la wakimbizi.

Akizungumza katika mji mkuu wa Senegal, Dakar waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amesema kuwa makubaliano hayo yamepiga hatua kubwa katika kudhibiti uhamiaji haramu.

Chini ya makubaliano hayo Ufaransa itaisaidia Senegal katika shuguli za kuweka doria kwenye pwani za nchi hiyo na pia kupambana na wafanya biashara ya kuwavusha watu mipaka kinyume cha sheria.

Wakati huo huo serikali ya Ufaransa imesema kuwa itawarahisishia wafanya bishara wa Senegal na wanafunzi ili waweze kupata visa za kuingia nchini humo.