1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DAKAR: Mkataba wa uhamiaji kati ya Ufaransa na Senegal

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9J

Ufaransa na Senegal zimetia saini makubaliano ya kuzuia watu kuhamia Ulaya kwa njia isiyo halali. Mkataba huo unarahisisha kuwapokea wanafunzi, wafanya biashara na wasanii nchini Ufaransa. Wakati huo huo watu wanaohamia Ufaransa kinyume na sheria wataweza kurejeshwa Senegal kwa haraka zaidi.Serikali ya Ufaransa vile vile itatoa kiasi cha Euro milioni 2.5 kwa miradi ya kilimo nchini Senegal ili wafanyakazi wapate kubakia huko. Mkataba huo ulipotiwa saini katika mji mkuu wa Senegal,Dakar,waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy alizungumzia kile alichokiita makubaliano yasio na mfano katika historia ya nchi hizo mbili.