1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Covid-19: EU yawataka wananchi wake kupewa chanjo ya mafua

Saleh Mwanamilongo
15 Julai 2020

Umoja wa Ulaya unahofia maambukizi ya magonjwa mawili ya COVID-19 na mafua kwa wakati mmoja wakati wa musimu wa mapukutiko.

https://p.dw.com/p/3fN7U
Frankreich Grippeschutzimpfung
Picha: Getty Images/AFP/P. Pochard-Casabianca

Umoja wa Ulaya unahofia maambukizi ya magonjwa mawili ya COVID-19 na mafua kwa wakati mmoja wakati wa musimu wa mapukutiko.Ikiwa chanjo ya mapema itapatikana,wananchi wa Umoja wa Ulaya watapewa chanjo dhidi ya mafua kwenye msimu huu wa joto.

Tume ya Umoja wa Ulaya imezionya nchi wanachama kuanzisha mapema chanjo dhidi ya mafua ili kuepusha msongamano wa wagonjwa wa mafua na Covid-19 kwenye hospitali wakati wa msimu wa mapuputiko.

Marekani inaripoti visa vipya 63,262 vya maambukizi ya Corona mnamo kipindi cha saa 24 ziliopita. Jiji la Tokyo, nchini Japan limeongeza hali ya tahadhari kutokana na ongezeko la visa vya maambukizi. Nchini Ujerumani idadi jumla ya visa inakaribia 200,000.

Iran imetangaza leo kwamba wahudumu wa afya 140 walifariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19, huku ikichukuwa hatua mpya ya vizuizi vya kiafya. Jumla ya idadi ya maambukizi nchini Iran inafikia watu 262,173.

Hatua ya mwisho ya majaribio ya chanjo ya Covid-19

Indonesien | Coronavirus | Surabaya | Java
Picha: picture-alliance/Zumapress/Sijori Images

Jumatano India inaripoti visa vipya zaidi ya 30,000 vikiwemo visa 582. Huku jumla ya visa ikikaribia milioni moja, viongozi wameweka upya hatua za kuwafungia watu kutoka nje kwenye maeneo kadhaa ya nchi hiyo.

Mamilioni ya watu wanakabiliwa na vizuizi vipya wakati maambukizi ya virusi vya corona yakiongezeka, lakini katika dalili moja ya matumaini, kampuni moja ya Kimarekani imesema itaanza hivi karibuni hatua ya mwisho ya majaribio ya chanjo ya ugonjwa huo.

Nchi nyingi duniani zimeweka upya hatua za kuwafungia watu kutoka nje pamoja na vizuizi ili kudhibiti maambukizi mapya, wakati idadi ya visa ulimwenguni ikipindukia milioni 13.2 na zaidi ya vifo 576,000.

Maeneo ya kanda ya Asia Pasifiki, ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa yamefanikiwa katika kupambana na janga hilo, yalitoa ushahidi mpya wa kitisho kikubwa ambacho bado kinawekwa na kirusi hicho.

Kampuni ya Kimarekani ya Moderna imesema itaanza hatua ya mwisho ya majaribio ya chanjo yake Julai 27, baada ya kupata matokeo ya kutia moyo katika majaribio ya awali. Kampuni hiyo inaongoza katika mbio za kutafuta chanjo ulimwenguni, na wakati utafiti wake ukipaswa kuendelea hadi Oktoba 2022,matokeo ya mwanzo yanatarajiwa kupatikana kabla ya muda huo.