1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cotonou: Watu wasiopungua 90 wameuwawa kufuatia ajali ...

26 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFpA

ya ndege nchini Benin-Afrika magharibi.14 wamesalimika .Juhudi za kuwaokoa wengineo zinaendelea katika fukwe za Cotonou.Kwa mujibu wa idara ya mawasiliano ya uwanja wa ndege mjini Cotonou,tatizo katika injini ya ndege hiyo pengine ndio chanzo cha ajali hiyo.Ndege hiyo chapa Boeing 727 ilikua njiani kuelekea Beyrouth.Matatizo yamezuka muda mfupi baada ya ndege hiyo kuruka.Imegonga paa la nyumba mjini Cotonou,ikaripuka na kuanguikia baharini.Wengi wa abiria wake ni raia wa Libnan waliotaka kurejea nyumbani kwaajili ya siku kuu za mwaka mpya.Ujumbe wa Libnan ukiongouzwa na waziri wa mambo ya nchi za nje Jean Obeid umewasili Cotonou hivi punde.