1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cologne yasema haina maambukizi mapya ya corona

Josephat Charo
4 Mei 2020

Klabu ya Cologne imesema Jumatatu (04.05.2020) duru ya pili ya vipimo kubaini maambikizo ya virusi vya corona kwa wachezaji na makocha imebaini hakuna mwenye corona katika timu hiyo.

https://p.dw.com/p/3bkWm
Bundesliga 1. FC Köln gegen Bayern München
Picha: Imago-Images/Sportfoto Rudel

Vipimo hivyo vilivyofanyika Jumapili, vilichunguzwa katika maabara huru kwa mujibu wa klabu hiyo na Jumatatu kikosi cha kocha Markus Gisdol kitaendelea kufanya mazoezi katika makundi.

Cologne ilisema siku ya Ijumaa kuwa watu watatu wangewekwa katika karantini baada ya vipimo kubainisha walikuwa wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona. Watu hao baadaye walitajwa kuwa ni wachezaji wawili na daktari wa timu hiyo.

Kitengo cha ligi kinachopanga ratiba ya mechi, DFL, imeandaa mkakati wa usalana na usafi huku ikitumia ligi kurrejea viwanjani bila mashabiki mwezi huu wa Mei. Hii inajumuisha vipimo vya mara kwa mara na wachezaji pekee ambao wamepimwa na kubainika hawana virusi vya corona mara mbili mfululizo wanaruhusiwa kufanya mazoezi na kucheza mechi.

Jumatano wiki hii kansela wa Ujerumani Angela Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo watakutana tena kujadili kulegeza vikwazo vilivyowekwa kuzuia kuenea kusambaa kwa virusi vya corona Ujerumani. Uwezekano wa kuiruhusu Bundesliga irejee tena ni suala lililpo katika ajenda ya mkutano huo.

(dpa)