1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

COLOGNE: Papa Benedict wa 16 atoa salamu kwa vijana wa kikatoliki na wasio wakatoliki

19 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEjj

Takriban vijana laki 4 wa kikatoliki kwa furaha na nderemo waliamkuana na papa Benedict wa 16 katika tamasha la vijana mjini Cologne magharibi mwa Ujerumani.

Papa Benedict wa 16 alidhihirisha furaha yake ya kuzuru nchi aliyozaliwa kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuliongoza kanisa katoliki mwezi Aprili.

Ziara ya papa Benedict katika mji wa Cologne ilikuwa ahadi ya aliyekuwa kiongozi wa kanisa katoliki marehemu Yohana Paul wa Pili kwamba angehudhuria tamasha hilo la vijana.

Kiongozi wa kanisa katoliki alitoa hotuba kutoka kwenye jahazi katika mto maarufu wa Rhine na alitumia nafasi hiyo kutoa salamu zake sio tu kwa vijana wa kikatoliki bali hata wale wasio wakatoliki.

Katika ziara yake ya siku nne mjini Cologne papa Benedict wa 16 atazuru sinagogi na vilevile atakutana na viongozi wa kiislamu nchini Ujerumani.

Tamasha la vijana linaendelea hadi siku ya jumapili ambapo papa Benedict wa 16 atalifunga tamasha hilo rasmi baada ya ibada ya halaiki.