1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kusini

China yatoa rai kufuatia madai Pyongyang imerusha makombora

5 Januari 2024

China imetoa wito wa kile ilichokiita "kujizuia" kutoka pande zote baada ya Korea Kusini kusema kuwa jirani yake Korea Kaskazini imerusha makombora karibu na visiwa viwili vya Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4at23
Korea Kaskazini ilifyetua zaidi ya makombora 200 karibu na visiwa vya Korea Kusini mnamo Januari 5.
Wakaazi wa mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul, wakitizama televisheni kwenye kituo kimoja cha treni ikionesha ufyetuaji wa makombora wa Korea KaskaziniPicha: Jung Yeon-je/AFP

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China Wang Wenbin amewaambia waandishi wa habari kuwa, kutokana na hali ya sasa Beijing inatumai kuwa pande zote mbili zitaendelea kuwa tulivu na kujiepusha kuchukua hatua ambazo huenda zikazidisha hali ya wasiwasi.

Wang ameongeza kuwa, China inafuatilia kwa karibu kinachoendelea katika rasi ya Korea.

Saa chache tu baada ya Korea Kaskazini kurusha makombora, jeshi la wanamaji laKorea Kaskazini kwenye kisiwa cha mpakani cha Yeonpyeong lilifanya luteka za kijeshi.