1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China yakasirishwa na hatua ya Marekani

6 Februari 2023

Wanajeshi wa Marekani wameondoa mabaki ya puto linaloshukiwa kuwa la kijasusi la China lililodunguliwa baada ya kuwepo katika anga la Marekani kwa siku kadhaa.

https://p.dw.com/p/4N8hX
Symbolbild Beziehungen USA China Fahne Flagge
Picha: daniel0Z/Zoonar/picture alliance

China imeonesha hasira kudunguliwa kwa puto hilo, ikisisitiza kuwa ilikuwa ndege isiyokuwa na rubani iliyokuwa ikichunguza hali ya hewa na ilipotea njia.

Naibu waziri wa mambo ya nje Chinaamesema hatua hiyo ya Washington imeathiri na kuharibu pakubwa juhudi za pande zote katika kuleta utulivu na kuimarisha ushirikiano.

Kugunduliwa kwa puto hilo kulisababisha kuahirishwa kwa ziara ya waziri wa mambo ya nje Marekani, Antony Blinken, ambaye alitarajiwa kuwasili mjini Beijing jana Jumapili.