China na Marekani zimeingia kwenye vita kali vya kibiashara.China inasema Marekani imepuliza kipyenga cha kufungua vita kubwa vya kibiashara duniani kwa kuchukua hatua ya kutoza ushuru mkubwa bidhaa zake za thamani ya dolla bilioni 34.Rais Trump asema yuko tayari kuongeza hata zaidi bidhaa za kutozwa ushuru za China ikiwa China itaendelea kuwa mbishi kwa kulipiza kisasi