1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

China, Japan na Korea zakubaliana kuzidisha ushirikiano

27 Mei 2024

Mataifa matatu yenye nguvu mashariki mwa Asia China, Japan na Korea Kusini leo yamekubaliana kuzidisha mahusiano yao ya kiuchumi na kufufua mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria.

https://p.dw.com/p/4gLPA
Viongozi watau kutoka Korea Kusina, Japan na China mjini Seoul
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida (Kushoto), Waziri Mkuu wa China Li Qiang (Kulia) na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol (Katikati) wakiwa kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mkutano wao huko Cheong Wa Dae mjini Seoul, Korea Kusini Mei 27, 2024.Picha: Yomiuri Shimbun/AP Images/picture alliance

Katika ujumbe wa pamoja walioutoa baada ya mkutano wa kilele mjini Seoul mataifa hayo matatu yamesisitiza dhamira yao ya kuwepo kwa Rasi ya Korea isiyo na silaha za nyuklia na suluhisho la kisiasa katika masuala kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini.

Mkutano huo wa kilele wa mataifa hayo matatu ulikuwa ni wa tisa, ila wa kwanza tangu Desemba 2019 kutokana na janga la uviko 19 pamoja na mivutano kati ya Korea Kusini na Japan.

Tangu wakati huo mahusiano baina ya nchi hizo mbili marafiki wa Marekani yameimarika.