1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China, Iran watoa mwito wa kuondolewa vikwazo vya Iran

16 Februari 2023

Rais wa China Xi Jinping na Ebrahim Raisi wa Iran wametoa mwito hii leo wa kuondolewa kwa vikwazo nchini Iran, kama sehemu muhimu ya makubaliano ya kimataifa yaliyokwama kuhusiana na mpango wa nyuklia wa Iran.

https://p.dw.com/p/4NZoC
China | Ehrenprofessur der Universität Peking an Ebrahim Raisi
Picha: Iranian Presidency Office/APA Images via ZUMA Press/picture alliance

Wakuu hao wamesema vikwazo vyote vinatakiwa kuondolewa kwa namna inayofaa ili kuhamasisha utekelezwaji kamili wa makubaliano hayo ya kimataifa ya mwaka 2015.

Raisi kwa upande wake amesisitiza kwamba Iran haitakubalina na hatua zinazoegemea upande mmoja,ukandamizaji na vikwazo, ambavyo kwa pamoja vinadhoofisha amani na maendeleo na kuvuruga mfumo wa ulimwengu.

Soma pia:China yapinga Marekani kuziwekea vikwazo kampuni zake
  
Wakuu hao wawili wametoa mwito huo katika taarifa yao ya pamoja, ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara ya Raisi nchini China. Xi aidha amekubali mwaliko kutoka kwa Raisi wa kuzuru Iran na kuahidi kufanya hivyo katika wakati muafaka.