1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Tanzania chamteua Mwinyi kuwania urais Zanzibar

10 Julai 2020

Chama tawala nchini Tanzania Chama cha Mapinduzi CCM, kimemteua waziri wa ulinzi nchini humo Dk. Hussein Mwinyi kuwa mgombea wake wa nafasi ya rais visiwani Zanzibar.

https://p.dw.com/p/3f6OF
Hussein Mwinyi
Picha: gemeinfrei

Dk. Mwinyi, ambaye ni mtoto wa rais wa awamu ya pili Al-Hajji Ali Hassan Mwinyi, amewashinda wagombea wengine waliofika katika mchujo wa mwisho, ambao ni waziri kiongozi wa zamani Shamsi Vuai Nahodha na Khalid Salum Mohamed.

Katika mchakato wa ndani wa uchaguzi, Dk. Mwinyi amepata jumla ya kura 129, ambazo ni sawa na asilimia 78.65, dhidi ya kura 16 za Nahodha na 19 za Khalid Mohamed.

Awali, kamati  ya Utendaji NEC, ilichagua majina matano na kuyawasilisha kwa kamati Kuu. Pamoja na watatu waliofika duru ya mwisho, wengine walikuwa Makame Mbarawa na Khamis Mussa Omar.