1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CHADEMA yazindua mikutano yake Kanda ya Ziwa Victoria

23 Januari 2023

Chama cha upinzani nchini Tanzania, Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kimezindua rasmi mikutano ya kampeni katika ukanda wa Ziwa Victoria ambapo mkutano wake wa kwanza ulifanyika jijini Mwanza mwishoni mwa juma na Jumatatu wako mkoani Mara.

https://p.dw.com/p/4MZqI

Mikutano hiyo imeanza siku chache baada ya Rais wa Tanzania kufuta tangazo la kuzuia mikutano ya kisiasa lililodumu kwa takribani miaka saba. Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe anaitumia mikutano hiyo kuhubiri maridhiano, siasa rafiki na kuepuka visasi ili kujenga taifa lenye umoja. Mwandishi wetu Dotto Bulendu amezungumza na mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kutaka kufahamu kwa undani zaidi ipi ni ajenda kuu ya chama hicho hivi sasa baada ya kujizolea sifa ya kuwa wakosoaji wakubwa wa ufisadi miaka iliyopita.