1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CANBERRA Ubalozi wa Indonesia nchini Australia wafungwa

1 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF85

Waziri wa mambo ya kigeni wa Australia, Alexander Downer, amesema kifurushi kinachoshukiwa kuwa na silaha ya kibayolojia kimesababisha kufungwa kwa ubalozi wa Indonesia mjini Canberra. Ameongeza kusema kwamba wafanyakazi wa Indonesia wasiopungua 22 wametengwa katika chumba maalumu hospitalini.

Downer anahisi kifurushi hicho kimetumwa kufuatia upinzani wa raia wa Australia baada ya mahakama moja nchini Indonesia kumuhukumu mrembeshaji raia wa Australia, Schapelle Corby, kifungo cha miaka 20 gerezani kwa makosa ya kuingiza kilo nne za bangi katika kisiwa cha Bali kutumia mfuko wa mashua yake ya kusafiria katika mawimbi. Downer amevilaani vitisho vya hivi karibuni vilivyotolewa dhidi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Indonesia.