1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Canada yatangaza kusitisha ofisi za kibalozi India

20 Oktoba 2023

Canada imetangaza kuwa itasitisha shughuli za balozi zake katika miji mbalimbali nchini India na kuwaondoa wanadiplomasia wake wapatao 41 baada ya serikali ya India kutishia kufuta kinga za kidiplomasia kwa maafisa hao.

https://p.dw.com/p/4Xohj
Indien Amritsar | Sikh-Proteste vor Goldenem Tempel
Maandamano ya kupinga mauaji ya Hardeep Singh Nijjar mjini Amristar, Punjab, India.Picha: REUTERS

Tangazo hilo lililotolewa Ijumaa (Oktoba 20) zinazihusu ofisi za kibalozi katika miji  zile zilizopo Bengaluru, Chandigarh na Mumbai.

Hatua hiyo inajiri huku kukiwa na mzozo wa kidiplomasia kati India na Canada kufuatia mauaji ya kiongozi wa kundi la Singasinga ambalo linataka kujitenga na India yaliyotokea mwezi Juni kwenye kitongoji cha Vancouver.

Soma zaidi: Canada yawaondoa wanadiplomasia 41 kutoka India

Mwezi uliopita, India iliitaka Canada kupunguza idadi ya maafisa wake wa kidiplomasia nchini mwake, baada ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau kuzungumzia kile alichosema ni ushahidi unaoonesha maafisa wa kijasusi wa India wanahusika na mauaji ya Hardeep Singh Nijjar, ambaye ni raia wa Canada.

Serikali ya India ilikuwa inanamuhusisha mwanaharakati huyo na ugaidi.