1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Canada: Kikosi maalumu cha jeshi la Iran ni cha kigaidi

Josephat Charo
20 Juni 2024

IRGC ni kikosi maalumu cha jeshi la Iran chenye majukumu ya kuilinda itikadi ya dola na juu ya yote, kuzuia mapinduzi. Kimekosolewa sana kwa kuhusika na ukandamizaji Iran.

https://p.dw.com/p/4hHLs
Vikosi maalumu vya jeshi la mapinduzi la Iran
Vikosi maalumu vya jeshi la mapinduzi la IranPicha: Iranian Army Office/ZUMA/picture alliance

Canada imekiorodhesha kitengo chenye ushawihi mkubwa cha jeshi la mapinduzi la Iran, Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC), kama kundi la kigaidi.

Waziri wa Canada anayeshughulikia masuala ya usalama wa umma, Dominic LeBlanc, amesema hatua hiyo inatoa ujumbe mzito kwamba Canada itatumia zana zote ilizonazo kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Waziri huyo aidha amesema serikali ya Canada itahakikisha kwamba hakuna kinga yoyote kwa hatua zisizo halali za Iran na msaada wake kwa ugaidi.

Soma pia: Umoja wa Ulaya kuliwekea vikwazo jeshi la walinzi wa mapinduzi wa Iran

Uamuzi huo una maana, pamoja na mambo mengine, kwamba ni kosa la uhalifu kwa mtu yoyote nchini Canada kukipatia msaada wa fedha au vifaa kitengo hicho cha jeshi la Iran na kwamba mali zake nchini humo zinatakiwa zizuiwe.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Israel Katz ameipongeza hatua hiyo.