1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Burkina Faso yawaua magaidi katika mashambulizi ya angani

8 Machi 2023

Kiasi ya magaidi 110 wameuawa nchini Burkina Faso katika kipindi cha siku chache wakati serikali ikiendelea kuyalenga makundi ya waasi kaskazini na kusini mwa nchi hiyo kupitia mashambulizi ya kutokea angani.

https://p.dw.com/p/4OOCa
Burkina Faso | Soldaten in Ouagadoudou
Picha: Kilaye Bationo/AP Photo/picture alliance

Kiasi ya magaidi 110 wameuawa nchini Burkina Faso katika kipindi cha siku chache wakati serikali ikiendelea kuyalenga makundi ya waasi kaskazini na kusini mwa nchi hiyo kupitia mashambulizi ya kutokea angani. Msemaji wa jeshi amethibitisha operesheni hiyo bila kusema idadi ya watu waliouawa mpaka sasa. Katika upande wa kaskazini mwa Burkina Faso, amri ya kutotembea nje usiku na marufuku ya kuendesha aina fulani ya pikipiki imekuwepo tangu wiki iliyopita.Amri ya kutotoka nje yawekwa Burkina Faso kupambana na ugaidi

 Serikali ya mpito ya Rais Ibrahim Traore, ambayo iliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi, mpaka sasa imeshindwa kuwarudisha nyuma wanamgambo hao. Karibu askari 70 waliuawa katika mashambulizi ya Februari katika siku chache. Kwa mujibu wa shirika la haki za binaadamu Burkina Faso Movement for Human and Peoples Rights, karibu raia 60 waliuawa wakati wapiganaji walikishambulia kijiji kimoja cha mkoa wa Tapoa mashariki mwa nchi hiyo mnamo Februari 26, na kuharibu mali na kupora mifugo.