1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBurkina Faso

Burkina Faso imemataka balozi wa Ufaransa nchini kuondoka

3 Januari 2023

Serikali ya kijeshi ya Burkina Faso imemtaka balozi wa Ufaransa nchini humo Luc Hallande kuondoka.

https://p.dw.com/p/4LhKv
Burkina Faso Ibrahim Traore Putschführer
Picha: Kilaye Bationo/AP Photo/picture alliance

Waziri wa mambo ya nje wa Burkina Faso Olivier Rouamba aliiandikia ofisi ya rais wa Ufaransa mwishoni mwa Desemba akitaka kubadilishwa kwa Hallade.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni chini ya wiki mbili baada ya Burkina Faso kumfukuza mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Barbara Manzi.

Mnamo mwezi Novemba, ubalozi wa Ufaransa mjini Ouagadougou uliishtumu Burkina Faso kushindwa kutoa ulinzi tosha kwa majengo yake yaliovamiwa wakati wa maandamano ya kuipinga Ufaransa mwaka iliyopita.