1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Ulaya lamtunuku Mahsa Amini tuzo Uhuru ya Sakharov

Hawa Bihoga
19 Oktoba 2023

Bunge la Ulaya limetanzaga kuwa tuzo ya Uhuru ya Sakharov ya mwaka huu itatolewa kwa mwanamke Mahsa Amini, aliyefariki akiwa katika kizuwizi cha polisi na vuguvugu la maandamano ya wanawake wa Iran.

https://p.dw.com/p/4XlAb
Mahsa Amini, msichana ambaye kifo chake kilizuwa maandamano makubwa nchini Iran, ametunukiwa Tuzo ya Uhuru ya Sakharov na Bunge la Ulaya.
Mahsa Amini, msichana ambaye kifo chake kilizuwa maandamano makubwa nchini Iran, ametunukiwa Tuzo ya Uhuru ya Sakharov na Bunge la Ulaya.Picha: DW

Rais wa Bunge hilo, Roberta Metsola, amesema wanaendelea kusimama kwa fahari na watu jasiri ambao wanapigania usawa, utu na uhuru nchini Iran. 

Mahsa Amini, ambaye alikuwa na umri wa miaka 22, alifariki dunia akiwa mikononi mwa polisi wa maadili, baada ya kuzuiliwa kwa madai ya kukiuka kanuni za mavazi.

Soma zaidi: Iran: Waandamanaji waadhimisha mwaka mmoja wa ukandamizaji wa vikosi vya usalama Zahedan

Kifo chake kilisababisha maandamano makubwa katika taifa hilo la Kiislamu.

Tuzo ya Sakharov imekuwa ikitolewa na Bunge la Ulaya tangu 1988 kwa watu binafsi na mashirika ambayo yamekuwa yakitetea haki za binadamu na uhuru wa kujieleza.

Mwaka jana tuzo hiyo ilitolewa kwa watu wa Ukraine kwa kutetea nchi yao dhidi ya uvamizi wa Urusi.