1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bunge la Namibia lajadili maridhiano na Ujerumani

9 Juni 2021

Bunge la Namibia limeanza kujadili makubaliano ya maridhiano ambayo Ujerumani iliomba msamaha kwa taifa hilo kutokana na mauaji iliyoyafanya wakati ilipokuwa ikiitawala zaidi ya karne moja iliyopita.

https://p.dw.com/p/3udIb
Namibia,  Windhuk Tintenpalast Parlament
Picha: imageBROKER/picture alliance

Kura hiyo inatarajiwa kupigwa siku chache zijazo, na kisha kusainiwa na mawaziri wa kigeni wa nchi zote mbili.

Waziri mkuu Saara Kuugongelwa aliwasilisha mpango wa makubaliano hayo na kueleza tathmini tofauti za umma kuhusu nakala hiyo, lakini akaongeza kwamba ni muhimu kuwa na umoja wa kitaifa.

soma zaidi: Maoni: Ujerumani yatambua mauaji ya halaiki ya enzi za wakoloni nchini Namibia

Zaidi ya miaka 100 baada ya Ujerumani kufanya uhalifu katika koloni lake ambalo sasa ni Namibia, serikali ya Ujerumani hatimaye iliyatambua mauaji yaliyofanywa dhidi ya jamii za Waherero na Wanama kuwa ya kimbari katika makubaliano hayo.

Ujerumani inakusudia kukiomba rasmi msamaha kizazi cha wahanga na imetenga euro bilioni 1.1 kuwasaidia kwa muda wa miaka 30 ijayo.