1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA:FDD kinadai rais Ndayizeye hafai kuongezwa muda wa kuingoza Burundi

22 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFKh

Chama kikuu cha waasi wa zamani wakihutu kimetoa wito kwa viongozi wa mataifa ya maziwa makuu wanaokutana hii leo nchini Uganda kutomungezea muda wa uongozi rais Domitien Ndayizeye pamoja na serikali yake ya mpito.

Chama cha Fdd kimesema rais Ndayizeye ni kipingamizi kwa amani na hivyo hastahili kubakia madarakani.

Msemaji wa chama cha FDD Karenga Ramadhan amesema tayari wamekwisha waandikia wapatanishi na viongozi wanohudhuria mkutano wa Kampala kuwaomba kutomuongezea muda wa uongozi rais Ndayizeye kufuatia kuwa kipingamizi cha shughuli za kutafuta amani pamoja na kufanyika uchaguzi. Na badala yake kuwataka wapatanishi kuipa Burundi kiongozi mwingine atakayeipeleka kuelekea uchaguzini.

Mkutano huo umekuja kufuatia kuongezeka kwa hali ya wasiwasi wa kimataifa na eneo la maziwa makuu, juu ya kusimamishwa kwa mpango wa amani ya burundi uliokuwa unalegalega kufuatia mzozo wa kutungwa sheria zinazoukosoa uchaguzi.