1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BUJUMBURA: Rais Nkurunziza asema ana ushahidi

15 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDC1

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema leo kwamba ana ushahidi dhidi ya washukiwa waliokuwa na njama ya kuipundua serikali yake.

Katika matamshi yake ya kwanza tangu watu tisa walipokamatwa mwezi mmoja uliopita, ikiwa ni pamoja na rais wa zamani, Domitien Ndayizeye, rais Nkurunziza amesema washukiwa wote watashtakiwa hivi karibuni.

Wakosoaji wanasema serikali ya Burundi alizusha madai ya mapinduzi ili iwatie mbaroni viongozi wa upinzani nchini humo.