1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Budapest.Maandamano nchini Hungary bado yaendelea kumshinikiza waziri mkuu.

21 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAO

Watu 16 walijeruhiwa na 62 kutiwa nguvuni mapema leo asubuhi katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji katika mji mkuu wa Hungary, Budapest.

Kiasi ya waandamanaji elfu kumi 10,000 wanaandamana kwa siku ya tatu mfululizo kumtaka waziri mkuu Ferenc Gyurchani ajiuzulu.

Karibu vichwa upara 80 waliokuwa sehemu ya waandamanaji hao nje ya bunge, walipambana na polisi na waandamanaji 12 kujeruhiwa.

Polisi wa kuzuia fujo ambao wameimarishwa zaidi, walilazimika kutumia hewa ya kutoa machozi kujaribu kuwatawanya waandamanaji hao.

Upinzani huo dhidi ya waziri mkuu Gyurchani mwenye umri wa miaka 44, ulianza baada ya kutamka kwamba, kuungama mbele ya wabunge wa chama cha Kisoshalisti mwezi Mei, kuwa alilidanganya taifa juu ya hali ya uchumi, ili aweze kuchaguliwa tena katika uchaguzi uliofanyika mwezi April.

Waziri mkuu huyo amekataa kujiuzulu.