1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Budapest. Wanazi mamboleo waandamana mjini Budapest wakipinga kutokea kwa mauaji ya maangamizi nchini Ujerumani katika vita vya pili vya dunia.

17 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMK

Zaidi ya wanazi mamboleo 100 wamefanya maandamano nje ya ubalozi wa Ujerumani mjini Budapest wakipinga sheria za Ujerumani zinazowalenga wale wanaokataa kuwa kuliwahi kuwa na mauaji ya maangamizi dhidi ya wayahudi wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia nchini Ujerumani.

Maandamano hayo yalifanyika wakati wa siku ya kumbukumbu ya mauaji hayo ya maangamizi nchini Hungary. Watu hao wenye msimamo mkali pia walidai kuachiwa huru raia wa Kijerumani, Ernst Zuendel, ambaye alikamatwa nchini Ujerumani mwezi uliopita kwa kukataa kuwa mauaji hayo ya maangamizi yaliwahi kutokea.

Kwa upande mwingine mamia ya watu katika mji mkuu wa Hungary wamefanya maandamano katika kile kinachoitwa maandamano ya maisha, kuwakumbuka zaidi ya Wayahudi nusu milioni wa Hungary ambao waliuwawa katika mauaji hayo ya maangamizi.