1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Brussels:Kofi Annan ataka majeshi ya Ulaya kushiriki huko Lebanon.

18 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG6L

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amesema kuwa anategemea mataifa ya Ulaya yatachangia jeshi katika mpango wa Umoja huo kuanzisha jeshi ili kwenda kumaliza mapigano huko kusini mwa Lebanon.

Annan aliyasema hayo baada ya mazungumzo yake na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso aliyeelezea ridhaa yao ya kuchangia jeshi hilo.

Waziri wa Mambo ya Nnje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmaier hata hivyo amesema kwamba bado hakuna uhakika wa umoja huo kushiriki katika mpango huo.